SportPesa yawashukuru Watanzania kwa kuwaunga mkono mwaka 2017, huku ikiahidi kuendelea kuleta mabadiliko chanya

Dar es Salaam, Tanzania –Kampuni ya michezo ya kubashiri ya SportPesa leo Januari 4, 2018 imewashukuru watanzania kwa kuwaunga mkono kwenye jitihada zao za kuendeleza michezo nchini kwa mwaka ulioisha wa 2017

SportPesa kupitia kwa Mkurugenzi wake wa Utawala na Utekelezaji, Ndugu Tarimba Abbas, imetoa shukrani hizo kwenye mkutano na wana habari uliofanyika kwenye hoteli ya Best Western jijini Dar es Salaam ambapo Ndugu Abbas ameelezea jinsi kampuni ilivyojipanga kuendeleza mikakati waliyoianza mwaka 2017.

“Hakika mwaka 2017 ulikuwa ni wa mafanikio makubwa sana kwetu kama kampuni na kwa moyo wa dhati kabisa nipende kuwashukuru watanzania kwa kutupokea na kuwa nasi bega kwa bega.

“Licha ya SportPesa Kenya kuacha kudhamini michezo nchini Kenya, sisi kwa upande wetu tumejidhatiti katika kuhakikisha tunaendeleza yale mazuri tuliyoyaanza mwaka uliopita ambapo tumekuwa na matukio mengi ya kusisimua kuanzia siku ya uzinduzi Mei 9 ukifuatiwa na udhamini kwa vilabu vya Simba, Yanga na Singida United lengo kuu likiwa ni kuboresha miundombinu ya soka kwenye vilabu vyetu.

Aidha Ndugu Abbas alienda mbali zaidi na kuwashukuru watanzania na vyombo vya habari kwa ujumla kwa ushirikiano mkubwa waliouonesha kwa kampuni hiyo kupitia ziara ya klabu ya Everton nchini sambamba na ujio wa nguli wa klabu ya Arsenal, Sol Campbell.

“Niwashukuru watanzania na wana habari kwa ujumla kwa ushirikiano mliotuonesha wakati wa ziara ya klabu ya Everton. Kitendo cha maelfu ya watanzania kufurika uwanja wa taifa kwenye mechi ya Everton dhidi ya Gor Mahia lilikuwa ni jambo la kutia moyo na sisi kama kampuni kwa kweli tumefurahi sana.”

Mkurugenzi huyo aliwaomba watanzania kuendelea kuiunga mkono kampuni hiyo ambayo imedhamiria kuleta sura mpya kwenye sekta ya michezo nchini sambamba na kubadilisha maisha ya mtanzania mmoja mmoja.

“Ninawaomba watanzania waendelee kutuunga mkono ili kwa pamoja tuweze kufikia malengo. Tumedhamiria kufanya mabadiliko makubwa kwenye sekta ya michezo na utaliona hilo kupitia mambo mbalimbali ambayo tumeyafanya mpaka kufikia sasa kuanzia kwenye soka la vijana, vilabu pamoja na marekebisho ya uwanja wa taifa ambayo yamegharimu zaidi ya Sh. BIlioni 1.4 za kitanzania.

“Lakini pia kupitia promosheni ya Shinda na SportPesa, tumeweza na tunaendelea kuyabadili maisha ya watanzania kupitia bajaji za TVS KING ambazo zinatolewa kwa siku 100 mfululizo na kila siku mshindi mmoja anajishindia bajaji yake, hivyo natoa rai kwa watanzania kuendelea kubashiri na SportPesa ili waweze kubadili maisha yao.” alisema.

SportPesa ndiye mdhamini mkuu wa vilabu vya Simba na Yanga pamoja na Singida United kwa nchini Tanzania na hivi karibuni wanaendesha promosheni kabambe ya kujishindia bajaji za TVS KING ambapo kila siku mteja mmoja anayeweka ubashiri kupitia SportPesa anajishindia TVS KING kwa muda wa siku 100 mfululizo na hadi kufikia sasa tayari washindi 71 wameshapatikana.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *