SportPesa yamkabidhi Noel zawadi yake ya Bajaj TVS King Deluxe

Mkazi wa Makambako(Timba) mkoani Njombe Noel Lazaro amekabiziwa bajaji aina ya TVS KING DELEXE katika eneo lake la kazi mkoani humo.

Mshindi huyo aliyejishindia bajaji kupitia promosheni inayojulikana kama SHINDA NA SPORTPESA inayoendeshwa na kampuni ya michezo ya kubashiri nchini ijulikanayo kama SPORTPESA LIMITED.
Akizungumza wakati wa mahojiano Noel Lazaro alisema “Kwanza kabisa nilianza kusikia kwenye mitandao,baada ya hapo nikawa naziona bajaji barabarani nikaanza kujiuliza hawa watu wanafanyaje hadi wanashinda, kuna mtu nilimuuliza ambaye alimuelekeza mtu hadi akashinda TVS KING baada ya hapo nikaanza kubet mpaka nikafikisha shilingi 13,000.

“Nilivyopata hiyo pesa nikaanza kucheza Jackpot kila wiki huku nikiendelea kubashiri na kutuma neno SHINDA baada ya kuweka ubashiri wangu”

” Baada ya muda nikapigiwa simu kama nimeshinda bajaji aina ya TVS KING DELUXE na baada ya hapo nikawataarifu washkaji zangu ambao hawakuamini na kudhani kuwa ni matapeli baada ya hapo nikawaambia kuwa jamani eeh bajaji yangu leo inakuja.

” Aisee mpaka sasa hivi siamini kama bajaji iko hapo mbele na ni yangu kuanzia sasa hivi,bajaji hii itanibadili maisha yangu kutokana na kwamba mimi sasa hivi ni baba wa familia nina mtoto mdogo khivyo maisha yetu yatabadilika na kupitia bajaji hii mwanangu ataishi vizuri”

Akizungumzia ushindi wa mumewe, Mke wa Noel Lazaro (Vumilia Sanga) alisema kusema ukweli baada ya kushinda mume wangu alikuwa halali kwa furaha iliyonayo na kila nikimuuliza anasema hadi bajaji yake aipate ndio atatulia, Leo ni siku ya furaha sana kwangu kwani bajaji hii inaenda kubadilisha maisha yetu sisi kama familia”alimaliza Vulimia

Kutoka upande wa SportPesa, Mkurugenzi wa Utekelezaji na Utawala Ndugu Tarimba Abbas alisema SportPesa kupitia promosheni hii ya SHINDA NA SPORTPESA imedhamiria kubadili maisha ya watanzania kutoka sehemu zote hapa nchini, hivyo basi tunakaribisha watu wote walio juu ya umri wa miaka kumi na nane(18) kujifunza na kucheza kwani sisi ndio kampuni pekee ambayo mara utakapopatia ubashiri wako na kushinda pesa yako huingizwa kwenye akaunti yajo ya SportPesa hapo hapo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *