SportPesa yadhamini Mashindano ya Michezo ya Wanafunzi Vyuo Vikuu

Kampuni ya michezo ya kubashiri SportPesa Limited imeingia makubaliano ya kudhamini mashindano ya michezo ya wanavyuo yajulikanayo kama SPORTPESA TUSA GAMES leo Jumanne katika ofisi zao zilizoko Masaki, Peninsula House Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari Afisa Uhusiano wa SportPesa Tanzania, Sabrina Msuya alisema” Kwa miaka mingi tumeona nchi za wenzetu zilizoendelea zikinufaika na vipaji kutoka kwenye mashindano ya vyuo vikuu ambavyo vimeweza kung’aa hadi kwenye ngazi ya timu ya taifa
Sote tutakuwa mashahidi jinsi ambavyo Ligi maarufu ya mpira wa kikapu ya Marekani ya NBA ilivyosheheni nyota kutoka ligi ya vyuo kama vile Stephen Curry na Kevin Durant

Lakini pia tusisahau wanasoka nguli duniani kwenye mpira wa miguu kama vile Didier Drogba, Arsene Wenger na Juan Mata ni wasomi ngazi ya Chuo Kikuu.

Kwa hiyo sisi SportPesa kama wadau wa maendeleo ya soka nchini, tumeona ni muhimu kudhamini mashindano haya ili tuweze kuvipa nafasi vipaji vilivyofichwa kwenye vitabu viweze kuibuka ili kuua ile dhana kuwa wasomi hawana vipaji vya ziada nje ya shule.”

Naye Mwenyekiti wa mashindano ya michezo ya wanavyuo Ndugu Wilson Mdegela alisema “Tusa inapenda kuwashukuru sana SPORTS PESA kwanudhamini wa mashindano ya vyuo vikuu 2017. Sportspesa wameonesha UZALENDO wa hali ya juu unaopaswa kuigwa na makampuni na watu binafsi ili kukuza vipaji vya vijana wetu.
Tunamshukuru Mkurugenzi na watenda kazi wote wa Sportspesa kwa moyo huo. “

Tunaomba ushirikiano na vyombo vya habari ili kuyapa thamani mashindano na kukuza UZALENDO”

Naye Mkurugenzi wa Shadaka Sports management, Nasry Msulwa alisema “Tunawezesha vijana kupitia michezo kwa kuandaa matamasha ya michezo ambayo huwapa vijana nafasi ya kuonyesha vipaji vyao na kuvumbua vipaji katika sekta ya soka.
Sisi kama SHADAKA tuko tayari kufanya kazi na makampuni ya aina yote ili kuendeleza sekta ya michezo Tanzania na kuvumbua vipaji vya vijana ili kujenga taifa lijalo” Nasry alimaliza

Mwakilishi kutoka Clouds Media Group Ndugu Gardener G Habbash alimaliza kwa kusema “Sisi kama clouds media group kwa kushirikiana na TUSA kupitia kauli mbiu yetu ya tunakufungulia dunia kuwa unachotaka, tumeona kuna umuhimu kuangalia upande wa wanafunzi wa elimu ya juu wenye talent kuinua kufikia ndoto zao.

Tuliona peke etu haitowezekana tukakataa kuwa kaa tumeamua kushirikia na nyinyi wadau wetu Sportspesa, TUSA na Azam katika kufikia hilo lengo.
“Tunakaribisha wadau wote wanahabari, wanamichezo na vilabu kutolea macho na masikio yao kuhamia dodoma ili kuona kitakacho tokea. Mashindano haya pamaoja na kupata promo ya clouds media bali pia yatarushwa moja kwa moja na Azam tv.”

Tamasha hili la michezo ya wanafunzi wa vyuo vikuu linatarajiwa kuanza tarehe 14 Desemba 2017 katika uwanja wa chuo kikuu Dododma(UDOM) na kuhusisha michezo kama mpira wa miguu, kikapu, pete, riadha pamoja na kuogelea na kuzinduliwa rasmi na Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Mh. Dr. Harrison Mwakyembe.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *