Siri ya Mourinho yavuja

Moja ya jambo lililojulikana kwa kocha wa sasa wa Manchester United Jose Mourinho,  ni kipindi wakati anaifundisha klabu ya Inter Milan alipoamua kuwataka wachezaji waende mazoezini Jumatatu  wakati wa usiku na sio asubuhi kama ilivyozoeleka.

 

Watu wengi walitamani kujua ni kwanini kocha huyo aliamua hivyo,  ila kwa siku za karibuni sababu ya Mourinho kufanya hivyo ilijulikana. Hayo yameelezwa na mshambuliaji wa zamani wa Inter, Ianis Zicu ambaye aliitumikia klabu hiyo kwa miaka sita.

 

Zicu alisema” Mourinho alitaka tufanye mazoezi usiku kutokana na tabia ya Maicon kulewa.Maicon alikua ni mwenye nguvu sana sema alikua akija mazoezini huku akiwa amelewa.

 

“Maicon alikua akija Jumatatu asubuhi huku akiwa amelewa hivyo basi Mourinho akaamua ni heri siku hio mazoezi yakawa usiku ili kila mtu awe na hali nzuri ya kuweza kufanya mazoezi”

 

Mourinho ambaye aliifundisha Inter Milan kuanzia mwaka 2008 hadi 2010 na kufanikiwa kubeba mataji kadhaa na timu hiyo ikiwemo klabu bingwa Ulaya kabla ya kuhamia Real Madrid.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *