Singida v Lipuli: Pointi tatu muhimu kwa kila timu

Ligi Kuu ya Tanzania Bara inarejea tena dimbani kuanzia Ijumaa hii baada ya mapumziko ya kupisha michezoya kimataifa ambapo timu ya taifa ya taifa ya Tanzania ilikua ugenini dhidi ya Benin mchezo uliomalizika kwa sare ya kufungana bao 1-1.

Singida United baada ya kwenda sare ya bila kufungana kwenye mchezo uliopita dhidi ya Mtibwa Sugar itakua nyumbani kuialika Lipuli. Ni mchezo ambao timu zote zinahitaji kupata ushindi ili kujiweka sawa kwenye msimamo wa ligi hio.

Singida United kwenye nafasi ya sita, baada ya michezo tisa imefanikiwa kujikusanyia pointi 14 sawa na Tanzania Prisons iliyo kwenye nafasi ya tano tofauti ikiwa ni mabao ya kufunga na kufungwa tu, kwani Singida inatofauti ya mabao 2 huku Prisons ikiwa ni moja zaidi ya Singida.

Lipuli ikiwa kwenye nafasi ya 7 baada ya kushuka dimbani kwenye michezo yake tisa, imejikusanyia pointi zake 13, inaonekana kutokua na safu nzuri ya ushambuliaji lakini safu yake ya ulinzi pia inaruhusu mabao kiasi kwamba imeshindwa kuwa na mabao ya akiba.

Ukitoa mabao ya kufunga na kufungwa kwenye kikosi cha Lipuli, jibu utakalolipata ni 1, hivyo basi huu ni mchezo ambao tunategemea Lipuli kuruhusu bao au kufunga bao, ni ngumu kujua lipi kati ya hilo linaweza kujitokeza kwanza.

Kikosi cha Singida United kimekua na ubora mkubwa kwenye eneo la kiungo, wachezaji wake Mudathir Yahya na Kenny Ally kwenye mfumo wa 4-2-3-1 hutengeneza ugumu mkubwa katikati ya uwanja huku wakimuacha kotinyo akicheza huru kwenye dimba la juu.

Selemani Matola, kocha wa Lipuli anahitaji kuzuia mbinu ya Hans van Pluijm ambae ni muumini mkubwa wa soka la kushambulia, mara nyingi hutumia sana soka la kushambulia kwa kasi kupitia pembeni ambapo Deus Kaseke hugeuka mwiba mchungu kwa timu pinzani.

Licha ya kusema kwamba anahitaji kuibuka na pointi tatu kwenye mchezo huo, kocha wa Lipuli, selemani Matola lakini haitakua rahisi kuchukua pointi tatu kutoka Singida kwenye mchezo huo, dakika tisini nyingine za mtihani kwa makocha wa timu zote mbili.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *