Simba yasaka kuendeleza mwanzo mzuri  

Simba itaikaribisha Kagera Sugar ikiwa na matumaini ya kuendeleleza mwanzo mzuri katika Ligi Kuu Kuu Vodacom Tanzania Bara. Pambano hilo la Ligi Kuu litachezwa siku ya Jumapili kwenye uwanja wa Taifa.


Baada ya kupata ushindi mfululizo kwenye mechi mbili, kocha Dylan Kerr atakuwa na matumaini Zaidi ya kuibuka na pointi tatu dhidi ya timu hio ya Kagera yenye kawaida ya kuisumbua Simba katika misimu ya hivi karibuni.

Mshambuliaji Hamisi Kiiza aliyetokea benchi kwenye mechi dhidi ya Mgambo na kufunga bao lake la pili msimu huu anapewa nafasi kubwa ya kuendelea kung’ara.

Msenegali Pape N’daw aliyecheza kwa dakika nne dhidi ya Mgambo anaweza kupewa dakika Zaidi dimbani ili kuzidi kuimarisha utimamu wake wa mwili baada ya kuwa nje ya uwanja kwa muda.

Abdi Banda ni nje ya shida na Jonas Mkude aliyekuwa majeruhi bado hajafikia kiwango stahili cha utimamu wa mwili kuweza kucheza hio kesho.

Kwa upande wa Kagera Sugar iliyo chini ya kocha Mbwana Makata, pambano hili linaweza kuwa gumu kwao kwa sababu ya uchovu wa kusafiri kutoka mji mmoja kwenda mwingine ndani ya muda mfupi.

Kagera Sugar ilisafiri hadi Mbeya na kuwafunga Mbeya City kwa bao 1-0. Siku ya Jumatano ilikuwa mjini Songea ilipopambana na kupoteza mechi dhidi ya wenyeji Majimaji.

Mshambuliaji wa zamani wa Simba, Adam Kingwande na mkongwe Paul Ngwai na Iddy Kulachi wanatarajiwa kuongoza safu ya ushambuliaji ya Kagera Sugar.

Msimu uliopita Kagera Sugar walishinda 1-0 jijini Dar katika duru ya kwanza ya msimu, wakati Simba walifanikiwa kulipa kisasi kwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 katika mechi ya marudiano iliyochezwa Shinyanga.

Kikosi cha Simba kilichoinyuka Mgambo 2-0 : Peter Manyika, Mohamed Hussen, Hassan Kessy, Murushid Juuko, Hassan Isihaka, Jaji Majabvi, Awadh Juma, Said Hamisi Ndemla (Pape N’daw 86′), Mussa Hassan Mgosi (Ibrahim Hajibu 67′), Mwinyi Kazimoto (Hamisi Kiiza 46′), Peter Mwalyanzi.

Wachezaji ambao hawakutumika: Angban Vincent, Emery Nimubona, Said Issa, Boniphace Maganga.

Yote tisa lakini kumi mpira unadunda tusubiri tuone kipi kitatokea katika mchezo huo.

Mechi za Jumapili za Ligi kuu ya Vodacom  

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *