Simba wakirekebisha haya ni moto wa kuotea mbali

Nimeitazama vyema sana jana Simba SC . Licha ya kucheza na timu dhaifu kimbinu na kiufundi lakini wameonesha wamejiandaa vyema kwa michuano hii ya kombe la Shirikisho.

HAMASA

Kila mchezaji aliyepata nafasi jana ya kucheza alikuwa na hamasa ya kusimama kama sehemu ya ushindi ama mafanikio kwa klabu yao. Hamasa hii ndio imewapa muunganiko mzuri kimbinu na kiufundi kitu ambacho kiliwafanya kutengeneza nafasi nyingi za kufunga na mwisho wa siku kupata goli 4.

MFUMO

Wingi wa viungo wenye uwezo mzuri wa kuchezea mpira kumeifanya Simba kuweza kuumudu vyema mfumo wao wa 3-5-2 unaohitaji wachezaji wenye skills nzuri kwenye dribbling, passing, Shooting and marking. Saidi Ndemla, Jonasi Mkude , Kichuya , Mlipili , Kotei , Kazimoto Okwi , Kwasi na Erasto Nyoni wote hawa wanatengeneza kombinesheni nzuri kwenye technical patterns za 3-5-2.

UFUNDI

Michuano hii ya kimataifa inahitaji umakini mkubwa sana wa kutumia nafasi ambazo timu inatengeneza ili kujiweka vyema katika ‘ mzingo ‘ wa mtoano. Simba wameonesha uwezo mzuri wa kutumia set pieces ambazo walifanikiwa jana kuzitengeneza . Upigaji wa faulo wa Saidi Ndemla ni jambo nzuri ambalo linachangia vyema uwezo wa timu kufunga katika njia zote.

Kosa kubwa ambalo linaonekana kwa haraka ni uwezo wa kupenya ngome ya wapinzani wao wakijaa kwenye marking zone yao. Kipindi cha pili Gendarmarie waliwasumbua sana kuvunja ngome yao kutokana na wahabeshi hao kufanikiwa kuziba njia za mpira .

Simba ndani ya 3-5-2 wanatakiwa kuongeza kasi kwenye ‘ direct play ‘ hususani njia ya kati kwa viungo wa kati kujenga link nzuri ambayo itawafanya wapinzani wao kurudi nyuma tactically imbalance.

Ukitazama kwa haraka kombinesheni ya Bocco na Emanuel Okwi kama jana ilitaka kukataa kwa Bocco kutembea sana eneo la mwisho huku Okwi mara nyingi akipata mpira anakuwa hatua moja mbele ya maamuzi hali iliyomfanya kupoteza nafasi nyingi kabla ya kusahihisha makosa yake mwishoni na kufunga kwa kusogea mbele ya lango. 3-5-2 inawapa nafasi washambuliaji wawili wa mbele ku overlap kulingana na nafasi ambazo viungo wa kati na wing men wanatengeneza . Bado namuona Okwi akitulia ataweza kuwa vyema na Bocco na kuipa timu magoli au kumtengenezea final passes nyingi Bocco.

Kiufundi kingine ni krosi za Wing backs Shomari Kapombe na Asante Kwasi . Muda mwingi hazikuwa na macho mazuri pia dribbling yao haikuwa na kasi kwenye wing hali iliyowafanya Gendamarie muda mwingi kusoma movements zao na kujiandaa kuzuia kabla hawajashambuliwa ( pre marking ) .

Simba ikisahihisha makosa yake hususani kujenga mashambulizi yanayohama kutoka box moja kwenye jingine kwa kasi ( tempo ) wana uwezo kushinda goli nyingi zaidi ugenini pia itakuwa nafasi nzuri katika muendelezo wa kunoa mfumo wao wa 3-5-2 kabla ya kukutana na timu zenye uwezo mzuri kwenye marking na kushambulia.

By SAMUEL SAMUEL
Happy Birthday Sam

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *