Simba mpeni muda Masoud Djuma

Simba muungeni mkono Masoud Djuma . Nawapenda sana makocha ambao husimamia maamuzi yako hata kama yana gharama. Licha ya ukali wa safu ya ushambuliaji ya Azam FC lakini bado Masoud ameendelea kusimamia maamuzi yake ya kutumia walinzi watatu nyuma akiamini atajilinda kwa kumiliki kiungo akiwa na viungo watano ambao ndio watapeleka pressure langoni mwa Azam ili kutafuta ushindi pia kuwaweka nyuma ya mstari.

Ni karata ya turufu kwake leo kama akifanikiwa kupata ushindi kwa Azam FC nadhani mnaompinga mtaanza kumwamini. Azam wamepoteza mchezo wa jana hivyo leo watacheza jihadi na ndicho wote tunakisubiri ili kuona ‘ tactical contact ‘ ya timu hizi ili kupata ubora halisi wa mfumo wa Masoud.

Hata kama atapoteza lakini pateni wasaa kufanya tathimini kwenye patterns zote ameshindwa na kufanikiwa kiasi gani ili kupata taswira ya ushiriki wa Simba kombe la Shirikisho na ligi kuuu kujaribu kulibeba kombe hilo kwa mara ya 19.

Wanafalsafa wanasema uoga mkubwa wa binadamu ni kukubali MABADILIKO .

Walinzi nyuma leo watakuwa Asante Kwasi kama mlinzi wa kati kushoto , Juuko Murshid kati na James Kotei kulia.

Viungo ni Mohamedi Hussein pembeni kushoto ambaye pia mbali na kusaidia mashambulizi atakuwa kama wing back ( defensive midfielder) , Mzamiru na Mkude watacheza ‘double six ‘ kati kuwalinda walinzi wa nyuma huku wakitengeneza daraja juu na Said Ndemla kama kiungo mshambuliaji/mchezeshaji ( deep lying playmaker) . Kichuya atacheza kulia kama kiungo mshambuliaji akisaidiana na Kotei kuilinda wing hiyo kwa mashambulizi ya upande ingawa pia Mkude anaweza kutanukia pembeni.

Gyan na John Bocco wakisimama kama washambuliaji .

Uwezo wa viungo watano wa kati na walinzi watatu nyuma ndio tegemeo la Simba leo .

 

By Samuel Samuel

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *