Simba kumkosa Ibrahim Hajib

Ibrahim Hajib

Ibrahim Hajib

Klabu ya Simba itateremka dimbani kuivaa JKT Ruvu katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara siku ya Jumatano bila ya mshambuliaji wake Ibrahim Hajib.

Hajib mwenye mabao sita mpaka sasa anatarajia kuukosa mchezo huo kutokana na kuwa majeruhi. Aliumia katika mchezo dhidi ya Mtibwa uliochezwa siku ya Jumamosi na Simba kuibuka na ushindi wa bao 1-0.

Hajib alipata maumivu eneo la uti wa mgongo yaliyomsababishia kupumzishwa mapema na nafasi yake kuchukuliwa na Danny Lyanga.

Mbali na kukosa pambano dhidi ya JKT Ruvu, Hajib ana hathati ya kucheza mechi ya mtoano wa Kombe la Shirikisho dhidi ya klabu ya Daraja la Kwanza, Bukina Faso siku ya Jumamosi mjini Morogoro.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *