Simba kuanza mazoezi Jumatatu ya kuikabili Singid United

Kikosi cha Simba SC kitaanza mazoezi yake rasmi siku ya Jumatatu kwenye viwanja vya Polisi Jijini Dar es salaam ,kuendelea kujinoa kwa ajili ya mechi za Ligi kuu Tanzania bara .

Simba inajiandaa na mchezo utakaofuata ambapo itakuwa mgeni wa Ndanda FC ya Mtwara.

Uongozi na benchi la ufundi ulitoa mapumziko ya siku saba! Kwa wale wachezaji wasiokuwa na majukumu ya kitaifa kwa maana ya uwakilishi wao kwenye michuano ya Chalenji inayoanza rasmi tarehe 3 December 2017 nchini Kenya.

Simba imenuia msimu huu kuibuka na ubingwa wa ligi kuu, ASFC, Mapinduzi Cup na kufika mbali katika uwakilishi wao wa kombe la Shirikisho barani Afrika michuano itakayoanza rasmi mapema mwezi February mwakani.

By Samuel Samuel

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *