Serengeti yadhamini Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania(TFF) na Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) Leo Jumatano Januari 10,2018 wamesaini mkataba wa miaka mitatu wa kuidhamini Ligi Kuu ya Wanawake (WPL) kupitia Bia ya Serengeti Lite mkataba wenye thamani ya shilingi milioni 450.

Hizi ni jitahada za TFF katika kuhakikisha mpira wa miguu kwa wanawake unachezwa kwa kuvisaidia vilabu kupunguza uchungu wa gharama za uendeshaji.

Katika historia ya soka la wanawake Tanzania, Serengeti wanakua wadhamini wa kwanza kujitokeza kudhamini soka la wanawake.

Ligi Kuu ya Wanawake inatarajiwa kuendelea kwa hatua ya 8 bora ( Super 8) baada ya kuchezaa kwa hatua ya kwanza ya makundi mawili yakiyoku na vituo Arusha na Dar es salaam.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *