Samatta atwaa tuzo ya mchezaji bora Africa

Mshambuliaji wa kimataifa wa Taifa stars na TP Mazembe ya JK ya Kongo Mbwana Samatta ameibuka mshindi wa tuzo mchezaji bora Afrika kwa kipengele cha wachezaji ndani ya Afrika katika sherehe Za Glo CAF Awards zilizofanyika nchini Nigeria.

Samatta alieingia kwenye kinyang’anyiro hicho Kwa kuongoza Klabu yake TP Mazembe kutwaa ubingwa wa Ligi ya mabingwa Afrika huku akipachika mabao saba amempiku Bagdad Bounedjah Na mchezaji mwenzake wa TP Mazembe kipa mkongwe Robert Kidiaba waliokuwa wakigombea tuzo hiyo.

 Samatta amevunja rekodi ya kuwa Mtanzania wa kwanza Na mchezaji wa kwanza Kutoka Afrika Mashariki kushinda tuzo hiyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *