Salah atwaa tuzo ya mchezaji bora Afrika

Shirikisho la soka barani Afrika CAF limemtangaza Mohamed Salah kuwa mshindi wa tuzo ya mchezaji bora wa Afrika kwa mwaka 2017.

Mohamed Salah wa raia wa Misri anayeichezea klabu ya Liverpool ya nchini England katika kinyang’anyiro hicho amewashinda gwiji wa Gabon anayeichezea Borussia Dortmund, Pierre Emerick Aubameyang na kiungo mwenzake wa Liverpool na timu ya taifa ya Senegal Sadio Mane.

Washindi wengine wa tuzo kwa usiku wa jana tarehe 4 Januari 2018 ni kama ifuatavyo;

-Mchezaji bora wa Kike Asisat Oshoala (Nigeria )
-Mchezaji bora kijana wa Mwaka ni Patson Daka (Zambia U20 & Red Bull Salzburg)
-Tuzo ya Kocha Bora wa Mwaka imeenda kwa Hector Cuper kocha wa Misri
-Klabu bora ya Mwaka ni Wydad Athletic Club ya Morocco
-Timu bora ya Taifa ya Mwaka ni Misri
-Timu bora ya Taifa kwa wanawake ni Afrika Kusini
-Kiongozi Bora wa Michezo wa Mwaka Afrika ni Ahmed Yahya wa Mauritania
-Tuzo ya gwiji bora wa imekwenda kwa Ibrahim Sunday.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *