Safari ya Ndemla, wakala asema kuna kitu ndani ya Simba

Said Ndemla

Wakala wa mchezaji Said Ndemla aliyetakiwa kuondoka nchini jana kuelekea Sweden kwenda kufanya majaribio kwenye klabu ya AFC Eskistuna, Jamal Kisongo anaamini kuna mambo yanawekwa sawa kati ya uongozi wa klabu hio na mteja wake.

Kisongo ameyasema hayo baada ya Ndemla kutosafiri hio jana huku taarifa kutoka Simba ikieleza kuwa kiungo huyo atasafiri siku ya Alhamisi kutokana na matatizo ya usafiri yaliyojitokeza hio jana na kuzuia safari yake ya nchini Sweden.

Kisongo amesema kwamba anaamini Simba wanaweka mambo ya kiuongozi sawa kabla ya kumruhusu huku akithibisha kwamba Ndemla alikua na kikao na raisi wa klabu hio licha ya kutoweka wazi yaliyokua yakijadiliwa kwenye kikao hicho.

Kiungo wa Simba, Saidi Ndemla. [Picha/Azamtv]

“Lazima tukubali kuna kitu ndani ya Simba kinawekwa vizuri, alikuwa na kikao na raisi wa Simba, mimi nasisitiza ni lazima tuheshimu hilo maana litakwisha tu,” alifafanua Kisongo.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka ndani ya Simba iliyothibishwa na Haji Manara ambae ndie Afisa Habari wa klabu hio, mipango ya safari ilimkwamisha Ndemla kutosafiri hio jana lakini safari yake ipo palepale na anatarajiwa kuondoka nchini siku ya Alhamisi.

Licha ya mabadiliko hayo, Ndemla hatoathirika na siku alizotakiwa kuwepo nchini Sweden akifanya majaribio ambazo zinatajwa kuwa ni siku 14, hio imethibishwa na Haji Manara.

“Ndemla ilikua asafiri leo, kutokana na mipango ya usafiri atasafiri Alhamisi, haiwezi kuathiri majaribio yake, Simba haiwezi kumbania mchezaji anapotaka kwenda nje ya nchi,” alisema Manara.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *