Roma v Chelsea: Miguu ya N’Golo Kante kuipa ushindi Chelsea?

Chelsea inashuka dimbani kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya, inaweza ikaendelea kujichimbia mizizi yake vema kileleni mwa Kundi C kwa ushindi dhidi ya Roma Jumanne usiku.
Timu hizo mbili zilimaliza mechi yao ya awali kwa sare ya 3-3 Darajani wiki mbili zilizopita, Chelsea inayoshika nafasi ya kwanza ikiwa imeizidi Roma pointi mbili.

Antonio Conte anaweza kuwa na N’Golo Kante kwenye kikosi chake baada ya kiungo huyo kuanza mazoezi Jumatatu, kufuatia majeraha aliyopata kwenye timu ya Ufaransa mapema Oktoba.

Bosi wa Chelsea alisema kundi lao ni gumu kwani Atletico na Roma ni timu mbili zinazoongeza ugumu kwenye kundi hilo.

“Kundi letu ni kundi gumu, Roma na Atletico Madrid ni timu mbili ngumu sana na kukaa kileleni ni muhimu sana.

“Wiki iliyopita tulifanikiwa kwenda raundi nyingine Kombe la Carabao, kisha tukashinda mechi mbili za mwisho Ligi ya Uingereza. Kwa hakika kesho [leo] itakuwa mechi ngumu kweli.

“Ni lazima tuwe makini sana kwa sababu Roma wapo katika kiwango safi.

“Ni muhimu kupita kipindi hiki kigumu kwa sababu wachezaji wetu muhimu wanarudi na nadhani mnafahamu ni muhimu kiasi gani kwangu kuwa na wachezaji wote.”

Conte amepanga kuongea na Kante kabla ya kufanya maamuzi ya mwisho kama atacheza Jumanne, na mechi yao dhidi ya Manhcester United ikiwa inakaribia.

Danny Drinkwater pia yupo tayari kuikabili Roma lakini Victor Moses ataendelea kukosekana akiuguza majeraha yake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *