Ratiba ya CAF kwa Ligi ya Mabingwa na Kombe la Shirikisho kutoka leo

Shirikisho la soka barani Afrika leo jumatano kuendesha droo ya michuano ya klabu bingwa Afrika na kombe la Shirikisho tayari kuanza kwa kipute cha msimu mpya wa 2018 mapema mwakani.

Yanga SC ndio wawakilishi wa Tanzania bara katika michuano ya klabu bingwa Afrika na Simba SC upande wa michuano ya kombe la Shirikisho.

Inatazamiwa michuano hiyo kuanza mapema mwezi February mwakani baada ya ratiba hiyo kutoka leo itakapochezeshwa nchini Misri katika jiji la Cairo yalipo makao makuu ya CAF.

Hatua ya awali upande wa michuano ya klabu bingwa Afrika itaanza kati ya February 9-11 na mechi za marudiano ni February 16-18.

Vilabu 16 ndivyo vitaingia hatua ya makundi kwa mfumo mpya wa CAF.

Ni zaidi ya miaka mitano sasa toka msimu wa 2012 ilikuwa mara ya mwisho kwa uga wa soka Tanzania kushuhudia wapinzani hawa wa jadi kuiwakilisha nchi kwa pamoja katika michuano ya CAF.

Orodha ya vilabu vya klabu bingwa Afrika vitakavyoingia katika droo ya CAF leo ni hivi hapa;

 

Algeria: Entente Setif, Mouloudia Alger, Angola: Primeiro Agosto, Benin: to be named, Botswana: Township Rollers, Burkina Faso: Kadiogo, Burundi: LLB Academic, Cameroon: Eding Sport, Central African Republic: Olympic Real Bangui, Congo Brazzaville: AC Leopards, Otoho, Democratic Republic of Congo: V Club, TP Mazembe, Egypt: Al Ahly, Misr Lel-Makkasa, Equatorial Guinea: Leones Vegetarianos, Ethiopia: Saint George, Gabon: Mounana, Gambia: Armed Forces, Ghana: Aduana Stars, Guinea: Horoya, Guinea-Bissau: Benfica, Ivory Coast: ASEC Mimosas, Williamsville, Kenya: Gor Mahia, Lesotho: Bantu, Liberia LISCR, Libya Al Tahaddy, Madagascar: CNaPS Sport, Malawi: Be Forward Mighty Wanderers, Mali: Stade Malien, Real Bamako, Mauritania: Concorde, Mauritius: Pamplemousse, Morocco: Difaa el Jadidi, Wydad Casablanca (holders), Mozambique: Songo, Niger: AS FAN, Nigeria: Plateau Utd, MFM, Rwanda: Rayon Sports, Senegal: Generation Foot, Seychelles: Saint Louis, South Africa: Mamelodi Sundowns, Wits, South Sudan: Wau Salaam, Sudan: Al Hilal, Al Merrikh, Swaziland: Mbabane Swallows, Tanzania: Young Africans, Togo: Port, Tunisia: Esperance, Etoile Sahel, Uganda: KCCA, Zambia: Zesco Utd, Zanaco, Zanzibar: JKU, Zimbabwe: Platinum

Samuel Samuel

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *