Rasmi: Wachezaji waliosajiliwa Yanga dirisha dogo

Justine Zullu ( Picha hisani )

Justine Zullu ( Picha hisani )

Dirisha dogo la usajili Ligi Kuu Tanzania Bara limefungwa usiku wa kuamkia leo ikiwa ni siku moja kabla ya kuanza kwa ngwe ya lala salama.

Kwa mujibu wa orodha ya TFF iliyowekwa mtandaoni, Bingwa mtetezi, Yanga wamefanya usajili wa wachezji wawili tu, mmoja wa kigeni, Emmanuel Joseph kutoka JKU ya Zanzibar pamoja na Justine Zullu kutoka Zesco United ya Zambia.

Yanga ilipata nafasi ya kumsajili kiungo mkabaji Zullu baada ya kuamua kutomuongezea mkataba kiraka Mbuyu Twite.

 

Kwa maana hio Yanga itaingia katika kampeni za Ligi ya Mabingwa Afrika ikiwa na ingizo moja tu jipya la Zullu kwani usajili mwingine unaweza kufanyika mwezi wa sita endapo watafuzu kwa hatua ya makundi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *