Promosheni Shinda Bajaj na SportPesa yazidi kunoga

NI miezi miwili sasa imepita tangu Kampuni ya kubashiri michezo nchini ya SportPesa-Tanzania kuzindua na kuendesha promosheni yake maarufu ya ‘Shinda na SportPesa’ ambayo imekuwa maarufu kutokana na kuchangamkiwa na watanzania wengi.

Promosheni hiyo ambayo lengo lake kubwa ni kuinua maisha ya watanzania kwa kugawa bajaji aina ya TVS King kwa wateja wao wanaoibuka washindi inaendelea kushika kasi.

Awali wakati wa uzinduzi wa promosheni hii, Mkurugenzi wa Utawala na Uwendeshaji wa Sportpesa Tanzania, Tarimba Abass alieleza dhumuni la kuanzisha kwa promosheni hiyo akisema ni kuinua vipato vya watanzania.
“Kuanzisha kwa promosheni hii lengo kuu ni kuona watanzania hususani wateja wa Sportpesa wanajikwamua kwa kujiongezea chanzo cha mapato kutokana na umiriki wa bajaji ambayo atashinda,” alisema Tarimba na kuendelea,..

” Promosheni yetu ilianza mwishoni mwa mwezi Oktoba na tunatarajia kupata jumla ya washindi mia moja hadi ifikapo mnamo mwanzoni mwa mwezi Februari mwakani”aliongezea kusema.

Tarimba alisema mpaka sasa wamefanikiwa kupata washindi kutoka sehemu mbalimbali za nchi na washindi hao wakiwa na kazi zao mbalimbali kama madaktari, walimu, maaskari, wanajeshi, waendesha pikipiki na bajaji pamoja na wafanyabishara wadogo wadogo.

Mpaka kufikia sasa zaidi ya wateja 67 wameshinda bajaji huku zikiwa zimesalia bajaji 33 ambazo zinaendelea kuwaniwa na watena wanaoshiriki katika promosheni hiyo.

Kauli za washindi
Baadhi ya washindi wa promosheni hiyo ambao tayari wamekabidhiwa bajaji zao, wameelezea namna walivyoanza kushiriki na kujikuta wanapigiwa simu za taarifa ya ushindi.

Musa Amir mwenye miaka 20 ni Mkazi wa jijini Mwanza, aliibuka mshindi katika droo ya 36 iliyochezeshwa Novemba 30 mwaka huu, anasema kuwa awali akuamini kama kuna uhalali katika promosheni hiyo.

“Awali nilikuwa siamini kama ni kweli, nilianza kushirki kucheza na baada ya siku chache nilipokea simu na kuambiwa nimeshinda, bado sikuamini mpaka pale nilipoletewa bajaji yangu,” anasema Amir.

Aidha, anasema kuwa bajaji hiyo imembadilishi maisha yake, akiwa bado mdogo tayari ana chanzo chake cha kumuingizia kipato kitakachomsaidia yeye na familia yake ikizingatiwa kuwa yeye bado mwanafunzi.

Naye Regan Zacharia, Mkazi wa Banda Mbili mkoani Arusha ambaye aliibuka mshindi katika promosheni ya 49, anaelezea namna alivyokabidhiwa bajaji yake akiwa ofisini kwake.

“Bajaji yangu imefika mpaka hapa, mimi sikutumia gharama yoyote na ukizingatia baada ya kupigiwa simu hakuna chochote nilichotoa zaidi ya taarifa zangu kwa ajili ya usajiri zaidi ya hapo kila kitu ni bure, Mimi nitaendelea kubashiri maana naona ninabahati sana.”

“Sitaacha kazi yangu ninayoifanya sasa hivi bali bajaji hii nitaitumia kwenye biashara zangu za kila siku ili iniongezee kipato”
“Kitu ndo kama hiki mnavyokiona ni kipya hata wewe unaweza kushinda hata kama sio bajaji unaweza shinda pesa na kilichosababisha ni hiki hapa ‘application’ ya SportPesa mpaka kupelekea ushindi wangu alimaliza Zacharia huku akionyesha bajaji yake na simu aliyotumia kubashiri.

Jinsi ya kubashiri na kushiriki promosheni ya Shinda na Sprortpesa

Afisa Uhusiano wa kampuni hiyo, Sabrina Msuya anaelezea namna ambavyo mtanzania anaweza akashiriki michezo ya Sportpesa na kushinda Bajaji yake mpya.

“Mtu yoyote anaweza kuwa mshindi kesho, unachotakiwa kufanya ni kutuma neno GAME kwenda 15888, kisha utafuata maelekezo yanayofuata, mara baada ya kuweka ubashiri wako kwa njia yoyote ile, unatakiwa kutuma neno SHINDA kwenda 15888 ili uweze kuingia kwenye droo ya kujishindia TVS Kinga Deluxe mpya kabisa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *