Preview: Mainz 05 v Hoffenheim 

Ijumaa hii katika Ligi Kuu ya Ujerumani ‘Bundesliga’ kutakuwa na mchezo mmoja kati ya Mainz 05 na Hoffenheim ambao utachezwa katika uwanja wa Coface Arena.

Mainz v Hoffenheim
Klabu ya Hoffenheim ambayo inashika nafasi ya 15 kwenye msimamo wa Bundesliga itakua ikisaka ushindi wao wa kwanza tangu msimu huu uanze baada ya kupoteza mechi 3 na kupata droo moja, Wapinzani wao wa ijumaa Mainz ambao wapo nafasi ya 10 wameweza kupata ushindi mara 2 dhidi Hannover 96 na Borussia Monchengladbach.

Mainz wameweza kupata ushindi mara 4 dhidi ya Hoffenheim, nao Hoffenheim wakipata ushindi mara 2, na kumekuwa na droo 4 katika michezo 10 ya Bundesliga iliyopita ambazo timu hizi zimekutana uso kwa uso tangu mwaka 2010.

Hoffenheim inayoongozwa na kocha mjerumani Markus Gisdol imeshindwa kupata ushindi katika mechi zake 10 za ugenini kwenye mechi 11 za Bundesliga zilizopita.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *