Pogba nje ya Uwanja kwa miezi mitatu

Kiungo wa Manchester United Paul Pogba huenda akakaa nje kwa miezi mitatu zaidi tofauti na taarifa za awali za wiki sita!.

Pogba aliumia dakika ya 18 tu ya mchezo wa klabu bingwa Ulaya dhidi ya Basle. Maumivu makali baada ya kuchanika nyama za paja ndio yalimtoa nje ya mchezo huo. Taarifa za awali zilitanabaisha anaweza kurudi uwanjani baada ya wiki sita lakini taarifa za leo jumapili ndani ya klabu hiyo kwa mujibu wa gazeti la Sunday times.

Taarifa zaidi zinaeleza kwamba sababu kubwa ya majeraha hayo ni mazoezi binafsi ya mchezaji huyo nje ya usimamizi wa benchi la ufundi la Manchester United, ushauri wa madaktari na wataalamu wa viungo wa klabu hiyo ambayo yamepelekea kumkakamaza misuli.

Wakati wowote kuanzia sasa mchezaji huyo anaweza kwenda nchini Marekani kwa matibabu zaidi kama alivyofanya mwanzo wa msimu.

Pogba anatazamiwa kukosa michezo mitano ya klabu bingwa Ulaya na michezo mitano ya ligi kuu dhidi ya Liverpool, Tottenham , Chelsea , Arsenal na Manchester city.

By Samuel Samuel

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *