Picha: Hii ndio zawadi ya Simon Msuva kwa Chicharito

Winga wa kimataifa wa Tanzania anaecheza soka nchini Morocco kwenye klabu ya Jadida, Simon Msuva ameonesha kuwajali na kuwakumbuka rafiki zake wa nchini Tanzania baada ya kuleta zawadi kwa moja kati ya rafiki zake hao.

Viatu na Jezi alivyokabidhiwa Godlistern Anderson Chicharito na Simon Msuva kama zawadi ya kumtakia heri kwenye siku yake ya kuzaliwa.

Msuva alimkabidhi zawadi ya jezi ya timu ya Jadida na viatu vya soka, aliekua Kaimu Afisa Habari wa Yanga, Godlistern Anderson Chicharito kwenye furaha ya kumtakia heri ya siku yake ya kuzaliwa.

Baada ya kukabidhiwa zawadi hio Chicharito alimshukuru winga huyo kwa kuonesha thamani kwenye siku yake hio muhimu huku akionesha kuifurahia zawadi hio.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *