Oscar atua Shanghai SIPG

oscarKlabu za Chelsea  ya Uingereza na Shanghai SIPG  ya China zimekubaliana juu ya uhamisho wa kiungo raia wa Brazil Oscar dos Santos Emboaba  Juniro (25) mapema ifikapo Januari 2017.

Kiungo huyo mshambuliaji wa Chelsea, Oscar atajiunga na klabu hiyo ya Shanghai SIPG kipindi cha usajili wa dirisha dogo litakapofunguliwa mapema mwakani mwezi Januari.

Oscar ameichezea Chelsea michezo 203 na kufunga mabao 38, ataanza maisha mapya China na klabu yake ya Shanghai SIPG mara dirisha dogo la usajili litakapofunguliwa.

Shanghai SIPG inayonolewa na aliyewahi kuwa kocha Chelsea mreno Andre  Villlas-Boas, inashiriki ligi kuu ya China (CSL) ambayo kwa sasa imekua maarufu kufuatia mastaa kibao kukumbilia kucheza ligi hiyo kwa ada kubwa za usajili.

Oscar anakuwa Mbrazil wa pili kujiunga na kikosi hicho, baada ya mshambuliaji Hulk aliyesajiliwa wakati wa dirisha kubwa la usajili akitokea klabu ya Zenit St Petersburg ya Urusi.

Baadhi ya wachezaji wenye majina makubwa wanaocheza ligi kuu ya China kutoka Afrika ni Demba Ba, Obafen Martins, Stephen Mbia, Gervinho, na Papiss Cisse,  huku America ya Kusini  wakiwepo (Ezequel Lavezzi, Ramires, Paulinho, Fernadinho, Carlos Tevez).

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *