Omog kaenda, Ila Simba ijitathimini

Siamini Joseph Omog alikuwa kikwazo cha maendeleo ya Simba SC. Ukitaka kutibu tatizo ni lazima uangalie mzizi wa tatizo husika na kuung’oa .

Toka 2012 Simba ilikuwa inachechemea kimbinu na kiufundi hali iliyopelekea kuingia mkataba na makocha si chini ya 7 na kuwafukuza kw akushindwa tu kufikia malengo stahiki ya timu. Malengo ni ubingwa ligi kuu, ASFC , Mapinduzi Cup na michuano mingine .

Omog kwa rekodi za haraka haraka tu toka aingie mkataba na Simba amefanikiwa kuwapa nafasi ya kucheza michuano ya kombe la Shirikisho kwa ubingwa wa ASFC huku akiukosa ubingwa wa bara kwa tofauti ya magoli na mabingwa Yanga SC kitu ambacho kilikuwa hakipo hapo mwanzo . Toka ujio wa Azam FC Simba walikuwa wanaishia nafasi ya 4 au ya 3 Premiere league.

Omog aliiwezesha Simba kucheza fainali ya Mapinduzi cup wakiwa katika kiwango bora licha ya kulikosa kombe mbele ya Azam FC.

Kwanini nasema Omog hakuwa kikwazo cha Simba katika maendeleo yao; toka msimu wa 2012 wakati Simba ikiwa katika ubora wake , hakuna kocha aliyeweza kufikia rekodi ya Omog.

Anabebeshwa zigo la kutolewa na Green Warriors katika michuano ya ASFC ilihali kwa zaidi ya wiki mbili timu alikuwa nayo msaidizi wake Masoud Juma. Huyu ndio aliyeiandaa timu kwa mchezo wa juzi lakini Omog akasimamia mchezo kama kocha mkuu. Jinsi Simba ilivyocheza na KMC ndivyo ilivyocheza juzi.

Timu si mbaya kwenye technical patterns, ina miliki mpira vizuri kosa dogo kwao ni kukosa plan B , kasi na hamasa ya kutafuta matokeo. Worriors walikaba Simba kutokana na mfumo wao wa kuhama box moja kwenda jingine hali iliyowapa kazi rahisi ya wao kuziba njia kwa kujituma katika kukaba na muda wote kuhakikisha hawaingii kwenye 18 yao kwa mpango uliosukwa vyema toka kati au pembeni.

Simba ijiangalie yenyewe katika mfumo wa usajili, kujenga hamasa ya wachezaji kuithamini jezi ya klabu hiyo.

Mara nyingi klabu hii wachezaji na makocha ambao kwa namba moja ama nyingine walipaswa kupewa muda , wameondolewa katika namna ambayo inashitua . Hili nalo walitazame maana kila mara mtakuwa mnaanza upya . Uondokaji wa Julio na Kibadeni, Kiiza , Tambwe , Bukungu , Mwanjali na kocha wa sasa Omog kunaleta ukakasi.

One Comment

  1. Lisungu Vincent mwela

    December 25, 2017 at 1:02 pm

    Usiangalie rekodi angalia uwezo wa timu uwanjan kwa wkt husika,Simba ikikutana na timu inayopaki basi haina ujanja,ndo mana walifungwa na vibonde Lyon lig iliyoisha,wakashindwa kuifunga Toto…km angeendelea hata vibonde wa Djibout wakija kupaki basi wangeweza kuizuia simba

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *