Okwi azidi kutakata Simba ikiichapa Mwadui

Ni kwa mara nyingine tena mshambuliaji wa Simba SC toka nchini Uganda anadhihirisha uwezo wake wa kucheka na nyavu baada ya kuondoka uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam akiwa na goli mbili Simba wakishinda 3-0. Goli la tatu la Simba lilitiwa kambani na John Boko.

Simba wakicheza kwa kujiamini na ufundi wa hali ya juu waliweza kulitawala pambano la leo kwa dakika zote 90 dhidi ya Mwadui FC ambao walionesha kupwaya toka dakika za mwanzo.

Joseph Omog akitumia mfumo wa 4-4-2 ; safu ya ulinzi wakisimama Mohamedi Hussein kushoto, Ally Shomari kulia kama walinzi wa pembeni na kati wakisimama Salumu Mbonde na mlinzi wa timu ya taifa ya Uganda Juuko Murshid ambaye alikuwa akicheza kama commanding central defender, waliweza kuidhibiti vyema safu ya ushambuliaji ya Mwadui waliojipanga kwa 4-5-1 na kujikuta muda mwingi wakicheza kwenye nusu yao.

Safu ya kiungo ya Simba SC kama kawaida iliongozwa na James Kotei akicheza kama kiungo wa chini. Leo Kotei alikuwa akicheza kama lone defensive midfielder akiwamudu vyema viungo wa Mwadui na kutawanya mipira atakavyo. Kiungo cha juu alisimama Mzamiru Yassin akicheza kama kiungo mchezeshaji na akiwaunganisha vyema Emanuel Okwi na John Bocco na kazi iliyokuwa ikianzia chini kwa Kotei au kwenye wings kwa walinzi Ally Shomari na Mohamedi Hussein ambaye leo amepata nafasi ya kuanza baada yakuwa nje katika mechi mbili za mwanzo.

Uwezo wa Simba kumiliki mpira kutokana na ubora wa viungo wake umewafanya Simba leo kucheza mchezo mzuri sana . Timu ilionesha kujenga mashambulizi kwa uhakika toka nyuma . Njia ya kati kuanzia kwa Kotei , Mzamiru kuja kwa Emanuel Okwi ilikuwa moto wa kuotea mbali. Ubora wa mganda huo kwenye dribbling na kuzifanyia kazi nafasi alizokuwa akipata na kutengeneza kumeifanya Simba leo kutakata taifa .

Mapema Okwi alitambua udhaifu wa beki ya Mwadui ambao walikuwa wanakatika na kuchelewa kuziba njia pia kipa wa Mwadui ambaye alikuwa akitoka bila hesabu nzuri kulimfanya Okwi kumfunga mara mbili kunako dakika ya 7 ya mchezo na dakika ya 68 kipindi cha pili pia dakika ya 72 Boko aliweza tena kuichachafya beki ya timu hiyo na kwa mtindo ule ule wa Okwi aliwafunga Mwadui ( semi volley ).

Nicholas Gyan wa Simba SC aliyechezeshwa kama kiungo mshambuliaji wa pembeni akitokea wing ya kulia kama angekuwa makini na yeye angeondoka na goli lake baada ya kukosa goli la wazi dakika ya 39 kipindi cha kwanza.

Mwadui wajilaumu wenyewe kupoteza mchezo wa leo. Hawakuwa na mipango mizuri ya kujilinda wala kushambulia. Muda mwingi walicheza kwenye nusu yao na walitegemea mashambulizi ya kushitukiza kusogea mbele. Licha ya kujilinda lakini walikuwa hawana muunganiko mzuri wa kujilinda hususani kuizuia kombinesheni ya safu ya ushambuliaji ya Simba iliyokuwa inaundwa na John Bocco kama mshambuliaji wa kati na Emanuel Okwi aliyekuwa akicheza kama deep playmaker akipewa ‘ back up nzuri’ na Mzamiru Yassin kati pia Shiza Kichuya kushoto.

Licha ya ushindi huo mnono lakini bado Simba ingeweza kutoka kifua mbele kwa idadi kubwa ya magoli kama wangecheza kwa kasi kama walivyocheza dhidi ya Azam FC au Ruvu shooting. Leo waliumudu mchezo lakini wakawa slow sio aggressive kama mechi zilizopita.

Simba imefikisha alama 7 kwenye ligi baada ya kucheza mechi 3 huku ikifunga goli 10. Ni Emanuel ndani ya kikosi hicho aliyefunga goli 6 kati ya goli hizo 10.

By Samuel Samuel

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *