Nyota wanne wa Bayern waongeza mikataba

Kama Kuna timu zilikuwa zinawanyemelewa basi itabidi watoe dau kubwa ili kuwasajili nyota hawa wa Bayern waliojifunga kwa mikataba minono. 

Javi Martínez, Thomas Mueller na Jerome Boateng wamesaini mikataba mipya itakayowaweka klabuni hapo hadi mwaka 2021.

Wakati kiungo mwenye macho ya Tai na mkali wa pasi ndefu Xabi Alonso yeye amesaini mpaka 2017.IMG_20151218_193500

Mueller alikuwa anahusishwa na mpango wa kuhamia Manchester United msimu huu lakini baada ya kusaini mkataba huo mpya amesema anayo furaha kuendelea kubaki klabuni hapo ambapo alijiunga tangu akiwa na umri wa miaka 11.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *