Niyonzima na binamu yake waiongoza Rwanda kuifunga Morocco

Djihad Bizimana akishangilia bao lake kwa staili ya kusujudu. ( Picha Hisani / NewTimes )

Haruna Niyonzima ambaye ni kiungo mchezeshaji wa mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga pamoja na binamu yake anayechezea APR, Djihad Bizimana waliisaidia timu yao ya taifa ya Rwanda kuifunga timu ya taifa ya Morocco kwa mabao 2-0.

Katika mchezo huo wa kirafiki wa kimataifa kuadhimisha kumbukumbu ya maadhimisho ya mauaji ya kimbari ya mwaka 1994, Rwanda ilipata mabao yake kupitia kwa Bizimana dakika ya 30 na Danny Usengimana kipindi cha pili.

Usengimana anaichezea klabu ya Polisi ya Ligi Kuu Rwanda na amekuwa akihusishwa na kujiunga na Singida United.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *