Ni wakati wa kunufaika na Rafiki Bonus kutoka SportPesa, Waalike marafiki wengi kucheza ujiongezee Kipato

Kwa siku za hivi karibuni uchumi umekuwa kikwazo kwa mtu mmoja mmoja hali ambayo imepelekea baadhi ya watu kufanya kazi nyingi zaidi ili kuhakikisha kuwa wanakuza mitaji yao.

Wapo watu ambao wanafanya kazi zenye kuwalipa kila mwisho wa mwezi lakini hufanya kazi nyingine pembeni ili kujipatia chochote kitu ndani ya siku husika. Hivyo ndivyo maisha yalivyo kwa sasa.

Michezo ya kubashiri nayo imechukua fursa yake kwa asilimia kubwa katika maisha ya watanzania hususani wale wapenzi wa soka ambao hutumia ujuzi wao wa kutazama mpira kujishindia donge nono.

Achana na kuweka mkeka wenye timu tano au zaidi na kushinda (multibet) au kucheza Jackpot kwa kubashiri mechi kadhaa kwa usahihi lakini pia fursa zimekuwa zikiongezwa kila kukicha na makampuni haya ya kubashiri ili kuhakikisha wateja wao hawakauki pesa mifukoni mwao.

Kwa wiki kadhaa sasa tumekuwa tukisikia promosheni ya Rafiki Bonus kutoka kwa kampuni ya SportPesa ambao ni wadhamini wa vilabu vya Simba, Yanga na Singida United.

Promosheni hii ina lengo la kumzawadia mteja wa SportPesa Sh 2000/= kwa kila rafiki anayemualika kujiunga na kucheza na SportPesa.

Mteja wa SportPesa anapaswa kumualika rafiki yake ambaye bado hajajisajili na SportPesa ili yeye aweze kushinda Sh 2000 na endapo ataalika marafiki kumi kwa siku basi mteja huyu anaweza kujikamatia kiasi cha Sh 20,000/= hivi hivi kiutani utani ingawa mwanzoni unaweza kuichukulia poa hiyo sh 2000 ukaiona ndogo.

Bila shaka hakuna tofauti kati ya bonasi hiyo ya Sh 2000 unayoipata na ile ambayo mawakala wa mitandao ya simu huipata kupitia wateja wanatuma pesa kwa simu zao na inaweza kuwa zaidi pia.

Faida za Rafiki Bonus
Kuna faida nyingi za kucheza Rafiki Bonus ya SportPesa na endapo kama ukiichukulia kwa umakini basi itakuwa ni chanzo chako kizuri cha kukuingizia pesa ya ziada ambayo usingeweza kufikiria kama ungeipata.
Kwanza ni rahisi: Hatua ya kucheza Rafiki Bonus ni rahisi sana kwasababu unachotakiwa kufanya ni kumwambia rafiki yako atume ujumbe mfupi kwenye simu yake wenye neno RAFIKI likifuatiwa na alama ya reli kisha namba yako ya simu uliyojisajilia SportPesa Mf. (RAFIKI#07XXXXXXXX) kwenda 15888 ambapo atakuwa ameshasajiliwa na atatumiwa ujumbe wenye jina la mtumiaji na namba yake ya siri.

Baada ya hapo rafiki yako ataweka pesa kwenye akaunti yake ya SportPesa kupitia M-Pesa, Airtel Money au Tigo Pesa kwa namba ya biashara/malipo 150888 ambapo namba ya kumbukumbu ni neno SPORTPESA.

Hatua inayofuata ni kucheza ambapo rafiki yako ataweka ubashiri kwenye mechi moja (single bet) ambayo odds zake zinaanzia 1.60 na kuendelea huku kiasi cha chini cha kubashiri kikiwa ni Sh 2000 Mf. (3547#2#2000) kwenda 15888 ambapo 3547 ni GAME ID, 2 ni utabiri na 2000 ni kiasi, lakini pia rafiki yako anaweza kucheza kupitia bet nyingi (multibet) au Jackpot na bado ukaweza kujipatia Sh 2000.

Muda mfupi baada ya rafiki yako kujisajili na kisha akaweka ubashiri wake basi utapokea ujumbe kutoka SportPesa ambao utakutaarifu kuwa umepokea Sh 2000 yako. Ni hivyo tu!

Pili, hakuna kikomo: Kucheza Rafiki Bonus hauwekewi kikomo cha idadi ya marafiki wa kuwaalika. Alika marafiki wengi kadri uwezavyo ii ujiongee mkwanja wako.

Tatu, Rafiki Bonus ina muendelezo: faida nyingine ni kuwa, wewe ambaye umealikwa na ukacheza halafu rafiki yako akapata bonasi pia unaweza kumualika rafiki yako na wewe ukapata buku mbili na rafiki yako uliyemualika anaweza kumualika rafiki yake akapata buku mbili kwa kufuata vigezo vile vile.

Nne, Unaweza kujiajili; Kupata Sh 20,000 kwa marafiki kumi uliowaalika kucheza rafiki Bonus ndani ya siku moja ni jambo kubwa sana katika uchumi wa sasa. Kama kwa siku moja umeweza kualika marafiki kumi ukapata Sh 20,000, ina maana kwa mwezi utaweza kualika marafiki 300 ambayo itakuwa ni Sh 600,000/= (laki sita) ambao ni mshahara wa mtu huo mwisho wa mwezi. Bado tu huamini kuwa inalipa?

Bila shaka utakuwa umepata maelezo ya kina jinsi ya kucheza Rafiki Bonus na utaanza kukamata fursa hiyo sasa kwani hutumii nguvu nyingi kuipata hiyo sh 2000/= bali ni nguvu yako ya ushawishi kwa marafiki zako tu ndio inahitajika.
Marafiki wengi, Mkwanja mrefu!
Kucheza na SportPesa inalipa!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *