Ni Jambo la Muda tu, Vijana hawa kulishika soka la nchini

Mshambuliaji wa Serengeti Boys, Yohana Mkomola

Ni jambo la muda tu Maka Edward, Said Mussa, RamadhanKawili na Yohana Nkomola kuwa muhimili wa ushindi wa timu ya Yanga na Taifa Stars.

Ni benchi la ufundi, marafiki hususani washauri wao wa karibu , dhamira yao ya ndani na wachezaji wakongwe ndani ya Yanga kuwajenga katika mtazamo chanya kisoka .

Ni zao jipya katika soka la nchi hii, matunda halisi ya kulea vijana yaani kuthamini soka la vijana ( Serengeti boys ) kwa mustakabali wa soka la nchi hii.

Hawa ni sehemu tu ya maelfu ya vijana wetu wenye vipaji vikubwa vya soka nchini ambao kama wanapitia njia sahihi ni lazima tuione ‘ Paradiso ‘ yetu kisoka.

Waingereza baada yakuona wanafeli katika soka hususani ngazi ya kimataifa , waliamua kukaa chini na kutafakari kitu gani wafanye ili wajikwamue katika hilo. Youth programs ndio suluhisho waliloliona na matunda yake yameonekana mwaka 2017 wakiwa mabingwa kombe la dunia chini ya umri wa miaka 17 na 20 huku timu yao ikifanya vyema katika kufuzu michuano ya kombe la dunia baadae mwaka huu nchini Urusi.

Vijana hawa na wengine wengi wasikatiwe tamaa bali kila uchao tufikirie njia sahihi ya kuwaendeleza. Always there is second chance tusimamie hapo sio wakikosea mara moja tunawaondoa katika ramani sahihi ya soka lao.

Tuwaongoze vyema katika mazoezi, elimi ya nadharia kisoka , masilahi yao na masuala mengine ya kinidhamu ili waje kuwa msingi wa soka letu.

Jana nilifanikiwa binafsi kuuona mustakabali sahihi wa nchi hii kisoka hususani Yanga . Klabu imekuwa ikitumia mamilioni ya pesa kusajili wachezaji toka nje ambao wengi wao huja hapa wakiwa katika magharibi ya soka lao. Lakini kikosi cha jana kimeonesha uwezo halisi wa klabu na nchi kuwasuka wachezaji wake ambao wanaweza kuwa bora zaidi ya hao.

Asanteni
🙏✍

By Samuel Samuel

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *