Ngoma apigwa STOP Yanga

Mshambuliaji wa Yanga SC aliyerejea hivi karibuni akitokea nyumbani kwao nchini Zimbabwe amepigwa marufuku ya kujiunga na wachezaji wenzake katika mazoezi ya pamoja mpaka hapo hatima ya hukumu yake itakapojulikana.

Ngoma anatuhumiwa na uongozi wa klabu hiyo kuiacha timu na kurejea kwao bila ruksa maalumu ya uongozi akidai alirudi nyumbani kwao kwa matibabu ya goti lake aliloumia kwenye mechi za awali za ligi kuu.

Wachezaji wa Yanga chini ya kocha msaidizi Shadrack Nsajigwa wameanza mazoezi ya Gym jumatatu hii kujiweka vyema na mechi nne zilizosalia za duru la mzunguko wa kwanza wa ligi linalotarajiwa kuanza tena baada ya michuano ya Chlenji inayofanyika nchini Kenya.

Ripoti ya mchezaji huyo kutoka kwa daktari wake uongozi umeiweka pembeni wakitaka ripoti kamili ya kitabibu kutoka kwa daktari wa timu pia hukumu ya kikao cha kamati ya utendaji kutokana na vitendo hivyo vya utovu wa nidhamu.

2 Comments

  1. Omary Jr Mfuko

    December 6, 2017 at 3:50 pm

    ikiwezekana afukuzwe ife fundisho kwa wengne

  2. kellah

    December 7, 2017 at 1:40 am

    mi nazani wanaomkumbatia Ngoma wana maslahi yao binafsi kuliko ya club, kwanini mchezaji anatusumbua yeye tu wakati Yanga ni kubwa kuliko brand ya MTU mmoja, mwacheni aondoke San it in I wachezaji WA club bingwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *