Ndoto za Geoffrey ‘Baba’ Kizito kucheza soka Hispania zaota mbawa, muda ndio kikwazo

Ndoto za kiungo wa timu ya taifa ya Uganda, Geoffrey ‘Baba’ Kizito za kucheza soka nchini Hispania zimeota mbawa baada ya kufeli kushindwa kufikishwa kwa dokomenti muhimu kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajiri barani Ulaya Jumatatu hii usiku.

image

Geoffrey 'Baba' Kizito.

Baba Kizito hana budi kusubiri kujaribu bahati yake kwa mara nyingine pale ambapo nafasi itatokea tena.

Ikumbukwe kiungo huyo alikuwa akifanya majaribio na timu ya Malaga CF inayoshiriki ligi kuu nchini Hispania, La Liga.

Kwa mujibu wa mtu anayehusika na masuala ya wachezaji, Rayco Garcia, kulikuwa na ucheleweshwaji wa karatasi muhimu zilizohitajika kwenda kwenye klabu ya Malaga kutokana na kutokuwepo kwa mjumbe wa Hispania nchini Uganda.

“Tumejaribu njia zote zinazowezekana na wameanua kupitia kwa mjumbe wa Ufaransa. Kwa bahati mbaya tumechelewa kutokana na kufungwa kwa dirisha la usajili”

Tayari Kizito alishafuzu changamoto nyingi na klabu hiyo ya Hispania kwenye mfululizo wa mazoezi na baadhi ya mechi za kirafiki alizocheza.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *