Ndanda yatua kwa Matola

Matola_

Baada ya kukosa timu ya kuifundisha kwa muda mrefu, kocha wa zamani wa Simba Selemani Matola huenda akajiunga na timu ya Ndanda kukiongezea nguvu kikosi hicho.

Ndanda wapo kwenye maandalizi ya mchezo ujao wa Ligi Kuu Bara chini ya kocha mkuu na uongozi wa timu hiyo upo mbioni kumsaka kocha msaidizi.

Taarifa rasmi kutoka kwenye uongozi huo zinaeleza kwamba tayari wana majina matano ya makocha waliotuma wasifu wao kutaka kuifundisha timu hiyo kama makocha wasaidizi.

Hata hivyo jina la Selemani Matola linaonekana kupewa nafasi kubwa ya kukinyakuwa kibarua hicho huku mwenyewe akikiri kuwa katika mazungumzo ya mwisho mwisho na viongozi wa timu hiyo.

“Tupo katika mazungumzo ya mwishomwisho, huenda nikajiunga nao” alisema.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *