Mwadui inakuja wakongwe, kaeni sawa

Wakati klabu kongwe za Simba na Yanga zikiwa bado zinahangaika kuutumia uwanja wa ‘jumuiya’ Mwadui wao wana Mwadui Complex uwanja wanaoumiliki wao wenyewe huko mjini Shinyanga.IMG_0993_20160321125806115

Ukiitazama Mwadui kwa jicho la tatu utaona jinsi Gani wanavyotamani mafanikio. Kama ilivyokuwa kwa Azam, Mwadui na wao azma yao ni kuhakikisha inang’ara zaidi kimataifa.

Haina mashabiki Wengi mikoani lakini kutokana na soka lao la Kuvutia limesababisha mashabiki wa timu pinzani kuanza kuwashangilia wao. Licha ya kocha wao kufahamika kwa maneno mengi Jamhuri Kihwelo almaarufu kama Julio Alberto Perreira amefanikiwa kufanya kitu ambacho makocha Wengi wazawa wanashindwa kufanya Kuiweka timu pamoja na kuweka usawa baina ya wachezaji wote.

Mwadui hakuna staa kumzidi kocha, na hili linafanya nyota wengine wa klabu za ligi kuu kutamani kujiunga na mwadui endapo watahitajika kufanya hivyo.IMG_1003_20160321125853502

kiungo mkabaji wa klabu ya Azam Fc Himid Mao aliulizwa swali wakati wa kipindi cha maswali na majibu kilichoendeshwa na mtandao wa www.soka360.co.tz Aliulizwa endapo ataondoka Azam je ni timu gani nyingine ya bongo anaweza kwenda? Himid alijibu ni Mbeya City au Mwadui.

Hii inaonyesha ni jinsi gani mwadui hakuna longolongo na ni moja ya Klabu chache ambazo husikii wachezaji wakinung’unika kutokulipwa au kucheleweshewa mishahara na posho zao
Jamani timu kubwa hamjachelewa igeni mfano wa kiuongozi kutoka kwa hawa jamaa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *