Mtibwa bado wanauota ubingwa

Unaweza kusema vichekesho. Timu ya Mtibwa Sugar ya Turiani, Morogoro bado inandoto za kutwaa taji la Ligi Kuu Tanzania Bara licha ya mwendo wa kinyonga uliyonayo timu hiyo.images-2.jpeg

 

Mtibwa Sugar ilipokea kichapo cha tano cha Ligi Kuu siku ya Ijumaa kutoka kwa ndugu zao Kagera Sugar na kuifanya isalie kwenye nafasi ya nne ikiwa na alama zake 39.

Hata hivyo  matumaini ya klabu hiyo kutwaa taji msimu huu huenda yakawa magumu kutokana na mwenendo wa timu tatu zilizojuu yake ambazo ni Simba waliopo kileleni wakijikusanyia alama 57, Yanga waliopo kwenye nafasi ya pili wakiwa na alama 50 sawa na Azam FC wanaoshika nafasi ya tatu tofauti ikiwa ni mabao ya kufunga na kufungwa.

Akizungumzia juu ya suala hilo Ofisa habari wa Mtibwa Sugar, Thobius Kifaru alisema licha ya kupoteza mchezo wao dhidi ya Kagera Sugar bado wanamatumaini ya kutwaa ubingwa.

“Matumaini bado yapo. Michezo iliyosalia kama wenzetu waliopo juu wakiteleza sisi si tunakuwa mabingwa!? Licha ya kupoteza dhidi ya ndugu zetu Kagera Sugar bado tunamatumaini ya kutwaa ubingwa”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *