Msuva apika bao la ushindi Difaa ikiizamisha FAR Rabat

Mshambuliaji wa Kimataifa wa Tanzania, Simon Msuva ameendelea kuwika katika Ligi ya Morocco kwa kuisaidia klabu yake ya DH Jadida kuibuka na ushindi wa ugenini wa mabao 2-1 dhidi ya FAR Rabat.

Msuva alihusika vilivyo katika ushindi hio kwa kupiga krosi murua iliyomaliziwa na mshambuliaji mwenzake Hamid El Ahadad katika dakika za nyongeza.

FAR Rabat walianza kufunga kupitia kw Mohamed El Fakih dakika ya 52, lakini Bilal Al-Makri akaisawazishia DH Jadida dakika ya 55.

Ushindi hio umewafanya DH Jadida kufikisha pointing 7 ikiwa ni pointing tatu nyuma ya vinara huku wakiwa na mchezo mmoja mkononi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *