Mshindi wa droo ya 57 akabidhiwa Bajaj yake na SportPesa Njombe

Mshindi wa droo namba 57 wa promosheni ya Shinda na SportPesa inayoendeshwa na kampuni ya SportPesa Nikorausi Sangu(34) akitokea Njombe, Makambako alikabidhiwa bajaji yake aina ya TVS KING wilayani humo.

Akizungumza juu ya ushindi wake Nikoraus alisema”Nafikiri ni kama mwezi mmoja na siku kadhaa hivi tangu nimeanza kubashiri kupitia SportPesa, huwa nacheza kupitia *150*87# na kwa siku huwa nacheza mara tatu.

“Kama wiki moja bivi mshindi kutoka makambako alikabidhiwa bajaji yake, nikamuomba anielekeze jinsi alivyojifunza mpaka kushinda bajaji aina ya TVS KING DELUXE”

“Leo mimi nimeshinda sikuamini maana usafiri naoumiliki ni baiskeli na kutokana na kazi yangu ya ufundi seremala kwa kipindi hiki kazi sio nyingi kama zamai, baada ya kushinda mtu wa kwanza kumpa taarifa alikuwa ni mke wangu maana amenivumilia sana kutokana na kazi zangu”

“Napenda kuwaambia vijana wenzangu wajifunza na waanze kubashiri na kampuni ya SportPesa ili kubadili maisha yao maana kama mnavyoona mimi nimebadili maisha yangu sasa hivi nitakuwa ni abiashara yenye kunipa uhakika wa kutokulala njaa, Uzuri wa SportPesa hauhitaji kusubiri baada ya kuweka ubashiri wako ni wewe tu hata ukiweka simu yako chini ya mto ukiamka kama umeshinda basi utakutana na ujumbe mfupi ukikutaarifu kwamba umeshinda na pesa imeshawekwa kwenye akaunti yako ya SportPesa”alimaliza Nikoraus

Akizungumza juu ya promosheni ya Shinda na SportPesa inayoendelea Mkurugenzi wa Utekelezaji na Utawala, Mr. Tarimba Abbas alisema “Mpaka sasa tumeshawatangaza washindi 69 kesho tunatarajia kumpata mshindi wa 70 ambapo tutabakia na washindi 30 mpaka kufikia tamati ya mashindano haya”

“Ningependa kutoa wito kwa wadau wa michezo na washiriki wa mashindano haya kuwa bajaji aina ya TVS KING hutolewa bila gharama yoyote na mshindi hatotumia kiasi chochote cha pesa mpaka atakapokabidhiwa bajaji yake, lakini kuna baadhi ya watu wanaosadikika kuwa ni matapeli wakiwashawishi watu watume kiasi cha fedha ili wawasaidie kupata ushindi, Watu hao ni matapeli na tunaomba endapo mteja wetu atapokea ujumbe kama huo tafadhali awasaliane na namba zetu za huduma kwa wateja ambazo ni 0764 115588, 0685 115588 na 0692 115588.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *