Mourinho humwambii kitu kwa Paul Pogba

Mourinho anamtaka Pogba kuendelea kuwa fiti ili kuendelea kuipaisha United –  na Mreno huyo anafahamu hilo.

“Pogba alikuwa juu,” Bosi huyo wa United alikiri baada ya mechi. “Ilikuwa kama vile hatoki kuuguza majeraha. Amerudi na kiwango kikubwa sana, mchezo wa kuvutia.

“Alipokuwa majeruhi niliamua kufunga mdomo wangu kwa sababu nadhani ndilo jambo jema ningeweza kufanya kwa wakati huo. Hatuwezi kulia-lia. Tunalazimika kucheza bila ya mchezaji fulani, ni budi kujaribu kutumia tulicho nacho.

“Lakini sote tunajua – mimi na wachezaji wenzake – kwamba baadhi ya wachezaji wanaamsha timu. Na amekuwa na athari kwenye mchezo wetu.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *