Mourinho badilika

Mourinho ameitengeneza Manchester United kuwa timu ya kujilinda muda wote. Huioni katika mtazama wa kushambulia muda wote. Uwezo mkubwa wa kushambulia humfanya mpinzani wako muda wote kurudi nyuma kuzuia hivyo kukupa nafasi nzuri ya kupanga mashambulizi na ku mshambuliaji pia unajitoa katika patterns za kuzuia kwa sababu muda mwingi opponent anakuwa chini ya mstari ( attacking zone ) akitegemea set pieces na counter kukushambulia.

Manchester city inapata matokeo mazuri kutokana na uwezo mkubwa wa kushambulia muda wote. Idara zote zimejipanga vyema kwenye defensive patterns and offensive patterns.

Jana Manchester United wametumia mfumo wa 4-2-3-1 Romelu Lukaku akicheza kama lone Striker mbele huku kati Paul Pogba na Nemanja Matic wakicheza ‘ double six ‘ . Automatically kwa mfumo wa 4-2-3-1 ni sawa na kucheza 4-5-1 . Ni mfumo ambao unalenga kujaza viungo wengi kati ili kuziba njia zote za mpira pembeni na kati (defense) .

Antony Martial kushoto na Juan Mata walikuwa wanacheza kama mawinga kujaribu kumchezesha Lukaku mbele ya walinzi wa Leicester ambao waliujua vyema mfumo wa Mourinho na kuamua kukabia juu huku viungo wao wakipasua ngome ya Manchester United ili mpira usikae kwao. Onyinye Ndindi na Vicente Ibora viungo wa Leicester city ambao pia walikuwa wanatumia 4-2-3-1 walijiweka vyema kuzima kasi za viungo na mshambuliaji pekee wa Manchester United ‘ Lukaku. Faida kubwa kwao ni Manchester kukosa kasi ya kushambulia kutokana na hofu ya ku unlock defense yao. Na hapo ndipo Mourinho anatakiwa kubadirika katika kujenga timu yenye ushindani.

Contact ya 4-2-3-1 kwa pande zote ina maana eneo la karibu lilikuwa na uwiano sawa wa wachezaji 1:1 kitu ambacho kimepelekea sare. Hii si sababu sana kiufundi ingawa inachangia pale mwalimu anapokosa mbadala wa mfumo wake.

FT ‘ Leicester city 2 Manchester United 2

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *