Mourinho aruka kihunzi Old Trafford

Kocha kuu wa klabu ya Manchester United baada ya mchezo wake wa klabu bingwa Ulaya dhidi ya CSKA Moscow alionekana mwenye furaha kufuatia ushindi wa goli 2-1 ulioiwezesha klabu yake kuingia hatua ya mtoana.

Ushindi huo umeifanya Manchester United kuingia hatua hiyo kwa mara ya kwanza toka msimu wa 2013-14 jambo ambalo linamfanya Mourinho kufanikiwa kuruka kihunzi ambacho kiliwashinda watangulizi wake.

Ilikuwa dakika ya 64 ya mchezo Paul Pogba akilishika vyema dimba la kati sambamba na Ander Herera alipomtengenezea pasi nzuri Romelu Lukaku ambaye bila ajizi aliwainua vitini mashabiki wa timu hiyo baada yakuwa wanyonge kutokana na CSKA kuwatangulia kwa goli la Vitinho dakika ya 45 kabla ya kwenda mapumziko.

Wakicheza kwa kujiamini, kasi , nguvu na hamu ya kushinda wakiwa nyumbani kwa mfumo wa 3-4-3 Manchester United walionekana mwiba mkali kwa CSKA Moscow dakika 20 za mwisho.

Juan Mata dakika mbili baadae baada ya Lukaku kuudhihirishia umma wa soka bado ni moto wa kuotea mbali katika kucheka na nyavu, Mata alimtengea vyema Marcus Rashford ambaye aliwapa Manchester United goli la pili na kumfanya mshambuliaji wa Everton Wayne Rooney aliyekuwa uwanjani akifatilia mechi hiyo kuinuka kitini kwa furaha kushangilia ushindi huo.

By Samuel Samuel

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *