Mourinho agoma kuwachezesha nyota wake wawili

Mourinho

Kocha mkuu wa klabu ya Manchester United, Jose Mourinho amesema hafikirii kuwapa nafasi ya kucheza nyota wake wawili hadi hatma yao ijulikane.

Nyota hao, Morgan Schneiderlin na Memphis Depay wanatarajiwa kutimka Old Trafford wakati huu wa dirisha dogo la usajili baada ya kushindwa kupata nafasi katika kikosi cha kwanza cha Mourinho.

Mourinho amedai kuwa kulikuwana uwezekano mkubwa wa wawili hao kuondoka lakini kwa sasa hana uhakika wa jambo hilo kutokea hivyo hawezi kuwajumlisha katika kikosi chake kinachojiandaa kucheza pambano la kombe la FA.

” Katika hali ya kawaida wangejumuishwa katika kikosi cha kesho lakini haijawa hivo kwa kuwa tunasubiri mambo ambayo wiki chache zilizopita yalikuwa yanaelekea kuwa asilimia 100 na sasa yanaonekana kuwa asilimia sifuri kutokea. Hatujapokea ofa zinazokaribiana na hadhi ya nyota tulionao.”

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *