Mkuu wa Wilaya Njombe, awakabidhi washindi wa droo ya 18, 19 Bajaj zao


Mshindi wa droo ya 18 katika Promosheni ya Shinda na SportPesa, Juviniki Edward Msambule (21) mkazi wa Makambako Iringa, akikabidhiwa pikipiki ya matairi matatu aina ya TVS King Dexule na mkuu wa wilaya ya njombe bi Ruth Msafiri.

Mshindi alionesha furaha kwa zawadi hiyo na kusema kuwa SportPesa imebadilisha maisha yake, kwani sasa anauwezo wa kuingiza kipato cha uhakika kila siku ukilinganisha na kazi yake ya awali ya ujenzi wa kujigemea ambayo haina uhakika wa kibarua cha kila siku.

Yusuph Ramadani (28) kutoka Makambako Iringa ndiye mshindi wa droo ya 19 katika promosheni ya Shinda na SportPesa iliyofanyika Novemba 13.

Mkuu wa Wilaya ya Njombe bi Ruth Msafiri akimkabidhi mshindi zawadi ya bajaji aina ya TVS King Deluxe aliyoipata baada ya kuweka ubashiri kupitia SportPesa. Mshindi anajishughulisha na ujenzi wa kujitegemea.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *