Mkali wa mabao Bundesliga, Pierre Aubameyang kuendeleza moto kwa Hamburger?

BUNDE
Baada ya kusimama kwa siku kadhaa kupisha michezo ya kuwania kufuzu kwa Kombe la Dunia, michezo ya kirafiki ya mataifa mbalimbali na kufuzu kwa Euro 2016, Ligi Kuu nchini Ujerumani inayojulikana kama Bundesliga inarejea dimbani ijumaa hii kwa mchezo mmoja kuvurumishwa.

Hamburger SV itawakaribisha Borrusia Dortmund ya Pierre Emerick Aubameyang, mchezo unaotarajiwa kuchezeshwa na mwamuzi Felix Zwayer.

Bundesliga imejizolea umaarufu mkubwa duniani baada ya Bayern Munichen “The Bavarians” kuonekana wapinzani wa kweli kwenye mbio za kugombania taji la Bundesliga.

Hata hivyo, ligi hiyo inachagizwa na matukio mbalimbali kama vile kiwango cha kushtusha cha wanandinga Robert Lewandowski na Pierre Aubameyang kutoka Gabon kutikisa anga la kabumbu duniani.

Pierre Emerick Aubameyang amecheza michezo 14 na Borrusia Dotmund huku akiweka kambani mabao 12, pia,ameisaidia Gabon kutinga katika hatua ya makundi kwenye michezo 9 mwaka huu ameweka kimiani mabao 5. Huenda akawa chachu ya ushindi kwa Borrusia Dortmund mbele ya Hamburger SV.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *