Migi kuigharimu Azam mamilioni

Jean Mugiraneza kushoto akiwa na mlinda mlango Aishi Manula ( Picha Soka360 )

Jean Mugiraneza kushoto akiwa na mlinda mlango Aishi Manula ( Picha Soka360 )

Aliyekuwa kiungo mkabaji wa Azam, Jean Mugiraneza amerudi nchini Tanzania kufuatilia haki yake baada ya kuvunjiwa mkataba na klabu hio ya Chamazi.

Migi alitemwa na Azam wakati wa dirisha dogo kwa madai amepata timu Vietnam habari ambazo alizikanusha na kuamua kusisitiza kuachwa kama mchezaji huru ili achague timu ya kwenda.

Haraka haraka alitua Gor Mahia ya Kenya na kusaini mkataba wa miaka miwili.

Juzi alirudi Dar kufuatilia haki zake za kuvunjwa kwa mkataba wake uliokuwa umebakiza miezi nane kumalizika.

Kwa mujibu wa mwandishi mmoja wa Rwanda, madai ya Migi yataigharimu Azam zaidi ya shilingi  milioni 40 kwa hesabu za mshahara wa milioni 5 kwa miezi nane.

Migi alisajiliwa mwaka jana akitokea APR ya nchini kwao Rwanda kwa mkataba wa miaka miwili na kuisaidia Azam kubeba kombe la Kagame.

Tayari Azam imemsajili kiungo wa Cameroon, Stephen Kingue kuziba pengo la Migi.

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *