Masoud Djuma akerwa na tabia ya Okwi

Kocha wa Simba, Masoud Djuma amemtaka mshambuliaji wa timu hiyo Emanuel Okwi kurejea nchini haraka na kujiunga na timu iliyopo Zanzibar ikishiriki michuano ya kombe la mapinduzi. Djuma amekerwa na staa huyo kutoka Uganda kushindwa kurejea kwa wakati na kuahidi kurekebisha nidhamu za wachezaji wa namna hiyo maana amegundua ni moja ya sababu zinazoifanya Simba kushindwa kufanya Vizuri.

“Naamimi Okwi atarejea ila sijajua ni lini, mara nyingi huwa sipendelei tabia kama hizi ndio maana nasisitiza nitaziondoa. wachezaji wajue majukumu yao ni yapi na sio kusujudiwa” alisema Masoud Djuma

-Okwi alikuwa majeruhi akapewa ruhusa ya kwenda kwao Uganda ila akaambiwa arejee mapema kabla ya mechi ya Ndanda ila Okwi alishidwa kufika muda huo akaombaa aongezewe muda ndipo uongozi ukamtaka aungane na timu huko Zanzibar kwenye michuano ya konbe la mapinduzi Cup ila mpaka leo (jana) bado Okwi hajajiunga na Timu hiyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *