Manchester United mpya na Lukaku ndani hii hapa

Romelu Lukaku ataongoza safu ya ushambuliaji ya Manchester United msimu ujao baada ya kukamilisha uhamisho wa pauni milioni 75 kutoka Everton. Usajili wa Lukaku umefuta mpango wa kumchukua Alvaro Morata kutoka Real Madrid.

 

Jose Mourinho alilazimika kufanya mabadiliko kidogo ya mfumo wa kikosi chake baada ya kuumia kwa Zlatan Ibrahimovic, hata hivyo Lukaku anafiti vizuri katika mfumo wa 4-2-3-1/4-3-3 unaopendelewa na mreno huyo.

Je, Mourinho ataongeza mshambuliaji mpya au ameridhika na silaha alizonazo? Ujio wa Lukaku utamuathiri vipi Marcus Rashford? kikosi Manchester United kitakuwaje msimu ujao?

Kuna uwezekano wa Mourinho kuendelea na mtindo wake wa kutumia mshambuliaji wa kati mmoja pamoja na kuwa alitumia washambuliaji wawili kuimaliza Chelsea msimu uliopita.

Inamaana Rashford atapelekwa pembeni kumpisha Lukaku afanye kazi katikati. Kasi ya Rashford itansaidia kushambulia akitokea pembeni.

Michael Carrick aliyetajwa kuwa nahodha mpya baada ya Wayne Rooney kuondoka hawezi kucheza mechi mbili kila wiki. United itahitaji miguu mipya kumsaidia Carrick.

Mourinho anachungulia uwezekano wa kumnasa mmoja kati ya Nemanja Matic au Tiemoue Bakayoko kuimarisha safu ya kiungo.

Ingizo jipya la Matic au Bakayoko litampunguzia majukumu Ander Herrera na kumruhusu kutembea zaidi huku Paul Pogba akipata uhuru wa kusogea mbele katika nafasi iliyomng’arisha akiwa Juventus.

Matteo Darmian hatazamwi kuwa suluhisho la kudumu katika nafasi ya beki wa kushoto licha ya kuwa kutokuwa fiti kwa Luke Shaw kunampa fursa ya kuwa katika kikosi cha kwanza mwanzoni mwa msimu mpya.

Henrikh Mkhitaryan anatarajiwa kumweka benchi Juan Mata kukamilisha ushirikiano wa washambuliaji watatu watakaoliamsha dude katika kikosi cha Mourinho.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *