Manchester City wanatumaini ujio Guardiola utamshawishi Messi

Klabu ya Manchester City inaamini kwamba ujio wa kocha Pep Guardiola utamshawishi mshambuliaji hatari wa Barcelona na timu ya taifa ya Argentina, Lionel Messi kujiunga na matajiri hao wa mafuta.

image

Licha ya kudhibitisha kwake juu ya kutokuwa na mpango wa kuihama FC Barcelona inaamini kwamba ujio wa kocha huyo mwenye mafanikio makubwa duniani utamvutia ikizingatia kwamba amekuwa na kashfa ya ukwepaji kodi.

Hata hivyo Manchester City italazimika kutoa kitita kikubwa cha fedha endapo itahihitaji kwa dhati huduma ya nyota huyo aliyetengeneza muunganiko mzuri na Luis Suarez na Neymar.

Lionel Messi aliwahi kukaririwa akikana kuwa na nia ya kuihama klabu ya Barcelona yenye maskani yake Katulanya.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *