Manara bwana, huu sasa ni utani wa ‘fimbo’

Bado yupo yupo sana! Ndivyo unavyoweza kusema baada ya Afisa Habari wa Klabu ya Simba, Haji Manara kuweka wazi matarajio yake ndani ya klabu hio.

Manara amesema kwamba anafurahia sana kuwepo ndani ya klabu ya Simba kwani ndio timu anayoipenda hapa Tanzania.

Matarajio ya Afisa Habari huyo ndani ya Simba ni kuendelea kusalia ndani ya klabu hio kwa miaka mingi zaidi huku akitania kuwa bado yupo yupo sana mpaka mwaka 2020.

Katika hatua nyingine Manara ameitetea klabu yake kwa kusema kuwa haina utaratibu wa kumzuia mchezaji wala mtu yeyote anapohitaji kwenda sehemu nyingine.

Huku akiongea kwa utani, Manara alisema hata leo hii akihitajika kuwa msemaji wa Manchester United anaamini Simba hawatamzuia.

“Simba haiwezi kumbania mchezaji, sio Ndemla tu hata mimi nikitakiwa kuwa msemaji wa Manchester United hawawezi kunizuia, lakini kwa sasa bado nipo Simba mpaka 2020, nafurahia kuitumikia klabu ninayoipenda,” alisema kwa utani Manara.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *