Man City yaiangamiza West Ham, Yaya Toure aendelea kutupia

Yaya_Toure Aguero

Kocha Pep Guardiola amefungua ukurasa wake wa kwanza wa Kombe La FA Uingereza kwa kuiongoza Manchester City kuiangamiza West Ham United kwa mabao 5-0. Ushindi huo umeipeleka Manchester City katika raundi ya nne ya Kombe la FA.

Yaya Toure aliipa bao la utangulizi Manchester City baada ya kuwamisha mpira kwenye Kamba kwa njia ya tuta mnamo dakika ya 33.

Baada ya kutangulia mbele, Manchester City ambao ni mabingwa mara tano wa kombe la FA waliendelea kuisulubu West Ham kwa mashambulizi hatari yaliyozaa mabao manne kupelekea wapinzani wao kupokea kipigo kikubwa Zaidi katika historia yao ya Kombe la FA.

Håvard Nordtveit alijifunga dakika ya 41 na dakika mbili baadaye David Silva akaongezea bao la tatu.

Iliwachukua City dakika tano tu za tangu kipindi cha pili kuanza kupata bao la nne lililozima kabisa matumaini ya West Ham kujikomboa. Sergio Aguero alimalizia mpira wa shuti kutoka kwa Yaya kufunga bao lake la 154 tangu ajiunge na matajiri wa City.

Bao la kichwa la Mlinzi John Stones lilihitimisha karamu  ya mabao kwa City mnamo dakika ya 84.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *