Man City v Burnley: City itaweza kuizuia Burnley isiguse nyavu zake? Bashiri sasa na Sportpesa

Sergio Aguero yupo fiti kuelekea kwenye mchezo dhidi ya Burnley hii leo, Vincent Kompany ataendelea kuwa nje akisumbuliwa na majeraha ya misuli wakati beki wa kushoto Benjamin Mendy anayesumbuliwa na maumivu ya goti atakosekana kwa muda mrefu.

Jonathan Walters anasumbuliwa na maumivu ya goti kwa upande wa Burnley,  Nahki Wells anasumbuliwa na maumivu ya mguu, pamoja na Dean Marney mwenye majeraha ya goti wote wanakaribia kupona vizuri, lakini bado wataendelea kuwa nje.

Licha ya kukosa ushindi kwenye mechi moja tu kati ya sita za Ligi ya Uingereza dhidi ya Burnley huku ikishinda mara 3 na kutoa sare mara 2, Man City wameshindwa kuwazuia Clarets kugusa nyavu zao.

Huu ni mwanzo mzuri kwa Burnley kwenye Ligi Kuu Uingereza baada ya mechi nane na kujikusanyia pointi 13, na mafanikio makubwa katika hatua hii ni tangu msimu wa 1973-74.

Manchester City wanapewa nafasi kubwa kutoka kifua mbele katika mchezo huu. Unaweza kubashiri kupitia Sportpesa, weka mzigo wako kwa kubonyeza hapa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *