Majimaji yawageukia mashabiki, hatarini kushuka daraja

Uongozi wa timu ya soka ya Majimaji kutoka mkoani Ruvuma imesema timu hiyo haiko katika hatari ya kushuka daraja msimu huu.

Mshambuliaji wa Majimaji, Danny Mrwanda

Mshambuliaji wa Majimaji, Danny Mrwanda

Akithibitisha hayo msemaji wa Timu hiyo maarufu wanalizombe Godfrey Mzira amesema timu hiyo itahakikisha inashinda mechi zake zilizosalia ili kuiwezesha kumaliza ligi katika nafasi nzuri.

“Kila mchezo kwetu ni fainali ili tuweze kupata alama nzuri ya kuepukana na balaa hili la kushuka daraja” alisema msemaji huyo.

Pia msemaji huyo amewaomba mashabiki na wapenzi wa Majimaji kujitokeza kwa wingi wakati wa mechi zao hasa za nyumbani ili kuwapa motisha.

“Niwaeleze mashabiki wa timu ya Majimaji kuwa sasa hivi tuko vizuri tunafanya vizuri na waendelee kutushangilia.”

Majimaji wako katika nafasi ya nane wakiwa na alama 27 baada ya kushuka dimbani mara 24 nyuma ya mbele ya Ndanda ikiwa na alama 25.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *