Mainz yaichapa Hoffenheim 3-1

Klabu ya Mainz 05 imenyakua ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Hoffenheim katika mchezo wa Ligi Kuu ya Ujerumani ‘Bundesliga’ ulio chezwa Ijumaa ndani ya dimba la Coface Arena.
Kiungo Mfaransa Jonathan Schmid alifunga bao mapema ndani ya dakika ya 13 akipokea pasi kutoka kwa kiungo Eugen Polanksi na kuiweka Hoffenheim mbele kwa bao 1-0.
Mainz walijibu mapigo dakika 5 baadae kupitia mshambuliaji wakijerumani Yunus Malli ambae alifunga bao la kusawazisha. Na mechi ikabaki sare ya mabao 1-1 hadi mapumzikoni.
Kwenye kipindi cha pili, Mainz waliendelea kuonyesha makali yao na straika Yunus Malli kudhibitisha kiwango chake cha juu alipofunga ‘hat-trick’ yake baada ya kufunga mabao mawili munamo dakika ya 61 na 68.
Malli mpaka sasa amefunga mabao 5 kwenye ‘Bundesliga’ akichukua nafasi ya 3 kwenye listi ya wafungaji bora mpaka sasa chini ya Pierre-Emerick Aubameyang wa Dortmund mwenye mabao 5 na Thomas Muller wa Bayern Munchen Mwenye mabao 6.
Kwa matokeo haya Hoffenheim wamepoteza mechi 4 katika mechi zao 5 waliocheza na kudidimia katika nafasi ya 3 kutoka chini, huku Mainz wakipanda hadi nafasi ya 3 kwenye msimamo wa ‘Bundesliga’ kabla ya Mechi za Jumamosi na Jumapili.

Mechi za Jumamosi hii kwenye Bundesliga

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *